Batarokota kulirudisha kundi la G tha Dunia


Pichani juu kushoto Batarokota akiwa na Cide Boy 

MKALI wa rapu nchini Tanzania ambaye ni mkurugenzi wa Batarokota Social Media, Paskal Linda a.k.a Batarokota, amedai anataka kulirudisha kundi hilo na kufanya shoo ya pamoja kwa ajili ya kumkumbuka nyota wa muziki huo, Notorious B.I.G. ambaye alifariki 1997.


Shoo hiyo inatarajiwa kufanyika Mei 21 ukumbi wa Brooklyn 44 Nairobi nchini Kenya, siku ambayo B.I.G alizaliwa, ambapo angetimiza miaka 44.


Mara ya mwisho kundi la G tha Dunia kufanya onyesho la pamoja ilikuwa mwaka 2002 kwenye Toure ya Tabora nchini Tanzania.“Hii itakuwa shoo ya kihistoria katika historia ya muziki wa hip hop ambapo wasanii wenye majina Bid d, Ngollo 2, Dj Zari wamealikwa,” alisema Batarokota.