Tanzania One Comic
burudani ya kipaji
Neyo, Diamondi, Batarokota kutumbuiza Jembeka Festival 2016!
MICHANO: DAZ BABA NAYE ANAHITAJI MSAADA KAMA CHID BENZI
YAP...yap...yap...Michano leo inamchana Daz Baba
mwanaharakati aliyetumbukia kwenye shimo la madawa ya kulevya, kiukweli
amepoteza mwelekeo ingawa kazi ni kazi ila inasikitisha pale
anapoendesha maisha yake kwakupiga debe kwenye vituo vya daladala.
Huyu
jamaa alikuwa kiongozi wa kundi kubwa na maarufu la muziki wa kizazi
kipya la Daz Nundaz lenye maskani yake Sinza Dar es Salaam, kundi hilo
lilijumuhisha wasanii watano akiwemo yeye.
Ila kwa sasa
kundi hilo halipo tena yaani kwa maana nyingine limekufa, Daz Nundaz
lilijipatia unaarufu mkubwa hasa kwa kuimba nyimbo za huzuni kama
Kamanda, Maji ya shingo, Barua na nyinginezo nyingi.
Aidha
Daz Baba binafsi amepata kutamba na nyimbo zake kama Elimu dunia, Umbo
namba 8, Wife, Nipe tano na nyingine, kwa sasa jamaa anahitaji msaada wa
kutupiwa kamba ili aishike na atoke kwenye shimo la madawa ya kulevya.
Kama
mmeweza kumpa kamba Chid Benz basi kamba hiyo mpeni na Daz Baba
kiongozi wa zamani wa kundi la Daz Nundaz lililojumuhisha vichwa kama
Ferooz Mrisho, Sajo, Larhumba, Critic na Daz mwenyewe.
Hata
hivyo inaonyesha tabia ya kuiga na kukata tamaa ndio chanzo cha
matumizi ya madawa ya kulevya, Michano inamshauri Daz Baba anapochoma
kuni asishangae majivu.
Tukutane Wiki ijayo kwenye
Michano inayojenga na si kubomoa inayotayarishwa na Rapa Mkola Man
mwenye chimbo lake Hale jijini Tanga, Ciao
Hongera Dk. Shein, lakini Zanzibar inahitaji umoja.
Katuni.
Uchaguzi huo ulifanyika kutokana na matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa
Oktoba 25, mwaka jana kufutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar
(Zec), Jecha Salim Jecha, kwa madai kuwa ulijaa kasoro kadhaa.
Hata hivyo, uamuzi wa Jecha ulikosolewa na makundi kadhaa wakiwamo
waangalizi wa kimataifa wakisema katika ripoti yao ya awali kuwa ulikuwa
mzuri kuliko hata wa mwaka 2010.
Chama cha wananchi (CUF) ambacho ni chama kikuu cha upinzani
Zanzibar kilipinga maamuzi ya Jecha na kutangaza kutoshiriki katika
uchaguzi wa marudio kwa kuwa kinatambua uchaguzi halali ni uliofanyika
Oktoba 25, mwaka jana.
Yanga wajipange kufuta uteja Al Ahly
Katuni.
Wanajangwani walishinda 2-1 ugenini jijini Kigali wiki mbili zilizopita kabla ya juzi kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani dhidi ya timu hiyo ya Jeshi la Rwanda.
Kabla ya kuivaa APR, Yanga iliikabili Cercle de Joachim ya
Mauritius na kuitua nje ya michuano hiyo mikubwa zaidi kwa ngazi ya
klabu barani kwa jumla ya mabao 3-0.
Kwa kutinga raundi ya pili, Yanga sasa itakuwa na kazi ngumu
itakapochuana na Al Ahly ya Misri kwa mara nyingine baada ya msimu
mmoja.
Timu hiyo ya Ligi Kuu ya Misri iliing'oa Yanga katika michuano ya
Afrika mwaka juzi katika hatua ya matuta baada ya kutoka sare ya 1-1
katika muda wa kawaida, kila timu ikishinda nyumbani.
Takwimu za soka zinaonyesha timu za Tanzania zimekuwa zikitolewa
mara nyingi kwenye michuano ya Afrika na timu za kaskazini mwa Afrika
(za Kiarabu). Kutokana na ukweli huo, Nipashe tunaona kuna haja Yanga
kufanya maandalizi ya kina kabla ya kuwavaa Al Ahly.
Timu za Kiarabu zinasifika kwa kuwa na mipango mizuri ya nje na
ndani ya uwanja katika kusaka matokeo. Yanga wanapaswa kujipanga
kikamilifu kuhakikisha wanadhibiti mianya ya fitna za Al Ahly.
Na kama kweli wamedhamiria kulipa kisasi cha matokeo mabaya ya
mwaka juzi, tunafikikri Yanga wanapaswa kuanza maandalizi mapema kabla
ya kukutana nao.
Licha ya kufanya vizuri katika raundi mbili zilizopita, tunaamini
kikosi cha Yanga kinakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zisizofanyiwa
kazi mapema, zitakuwa na athari kubwa mbele ya nyota wa Al Ahly
wasiofanya makosa mengi wanapokuwa na nafasi ya kuifunga timu pinzani.
Katika mechi mbili zilizopita dhidi ya APR, kwa mfano, Yanga
imeruhusu mabao mawili na safu zake zote kuanzia ulinzi hadi
ushambuliaji zilionekana kuyumba.
Tunafahamu kuna changamoto ya kuwa na majeruhi kadhaa kikosini,
lakini Yanga ilisajili nyota 24 kwa ajili ya msimu huu ambao tunaamini
wakielezwa mbinu chafu na fitna za timu za Kiarabu, wanaweza kutinga
robo-fainali kwa kuing'oa Al Ahly na kuiwakilisha vyema Tanzania msimu
huu.
Al Ahly iliyoanzishwa Aprili 24, 1907 (miaka 28 kabla ya Yanga
kuanzishwa), ina rekodi nzuri katika mashindano ya Afrika, Timu hiyo
imeshinda mataji nane ya Ligi ya Mabingwa na moja la michuano ya Kombe
la Shirikisho.
Tunafahamu pia kuwa Al-Ahly ndiyo timu namba moja duniani kwa
kushinda mataji mengi ya kimataifa (Klabu Bingwa duniani) wakifanya
hivyo mara 20 na kuzipiku AC Milan, Real Madrid na Boca Juniors.
Lakini mpira unadunda, Yanga walikaribia kuing'oa mwaka juzi, tunaamini wanaweza kupata mafanikio hayo mwaka huu.
Ndiyo maana tunatoa rai kwa uongozi wa Yanga na benchi lao la
ufundi kujipanga vyema ili kupata matokeo mazuri nje-ndani dhidi ya timu
hiyo
SOURCE:
NIPASHE
Kwa aina hii ya maandalizi, medali Olimpiki ndoto
Michuno hii mikubwa ya kimataifa, hufanyika mara moja kila baada ya miaka minne na kushirikisha mataifa mbalimbali duniani.
Zaidi ya michezo 50, ukiwamo soka hushindaniwa kwenye mashindano haya ya pekee na aina yake.
Tanzania ni moja ya nchi zinazotarajia kupeleka wawakilishi watakaoshindana katika michezo hiyo.
Ingawa kuna michezo zaidi ya 50 inayoshindaniwa, Tanzania itapeleka wawakilishi katika michezo mitatu; Judo, riadha na kuogelea.
Hata hivyo, pamoja na Tanzania kutuma wawakilishi kwenye mashindano haya kila yanapofanyika, bado hakuna mafanikio ya kujivunia.
Sababu kubwa ambayo imekuwa kama wimbo kwa Tanzania kushindwa kupata mafanikio ni maandalizi duni.
Maandalizi ya zima moto kwa wanamichezo wetu katika mashindano mbalimbali, ndiyo kiini cha kushindwa kufanikiwa.
Kwa wenzetu wanaopenda mafanikio na ndiyo ambao leo wanaendelea kufanya makubwa katika mashindano ya kimataifa, hujiandaa mara tu mashindano ya awali yanapomalizika.
Hawana muda wa kusubiri hadi mashindano yanapokaribia ndipo waanze maandalizi kama tunavyofanya sisi.
Katika hali ya maandalizi ya aina hii, hatuwezi kupata mafanikio. Pengine sifa kubwa itakuwa ni ushiriki usio na tija.
Azam, Yanga kazi haijaisha Afrika.
Katuni.
Yanga iliyokuwa ugenini kwenye Uwanja wa Amahoro jijini Kigali,
Rwanda, iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji APR FC katika
mechi ya kwanza ya Raundi ya Kwanza ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika.
Azam FC walichomoza na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Bidvest
Wits mjini Johannesbrug, Afrika Kusini katika mechi yao ya kwanza ya
Raundi ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho.
Wawakilishi pekee wa Zanzibar waliosalia kwenye michuano ya Afrika
mwaka huu, JKU FC wakitandikwa magoli 4-0 dhidi ya SC Villa ya Ligi Kuu
ya Uganda na kufifisha ndoto zao za kutinga Raundi ya Pili ya michuano
ya Kombe la Shirikisho.
Subscribe to:
Posts (Atom)



