YAP...yap...yap...Michano leo inamchana Daz Baba
mwanaharakati aliyetumbukia kwenye shimo la madawa ya kulevya, kiukweli
amepoteza mwelekeo ingawa kazi ni kazi ila inasikitisha pale
anapoendesha maisha yake kwakupiga debe kwenye vituo vya daladala.
Huyu
jamaa alikuwa kiongozi wa kundi kubwa na maarufu la muziki wa kizazi
kipya la Daz Nundaz lenye maskani yake Sinza Dar es Salaam, kundi hilo
lilijumuhisha wasanii watano akiwemo yeye.
Ila kwa sasa
kundi hilo halipo tena yaani kwa maana nyingine limekufa, Daz Nundaz
lilijipatia unaarufu mkubwa hasa kwa kuimba nyimbo za huzuni kama
Kamanda, Maji ya shingo, Barua na nyinginezo nyingi.
Aidha
Daz Baba binafsi amepata kutamba na nyimbo zake kama Elimu dunia, Umbo
namba 8, Wife, Nipe tano na nyingine, kwa sasa jamaa anahitaji msaada wa
kutupiwa kamba ili aishike na atoke kwenye shimo la madawa ya kulevya.
Kama
mmeweza kumpa kamba Chid Benz basi kamba hiyo mpeni na Daz Baba
kiongozi wa zamani wa kundi la Daz Nundaz lililojumuhisha vichwa kama
Ferooz Mrisho, Sajo, Larhumba, Critic na Daz mwenyewe.
Hata
hivyo inaonyesha tabia ya kuiga na kukata tamaa ndio chanzo cha
matumizi ya madawa ya kulevya, Michano inamshauri Daz Baba anapochoma
kuni asishangae majivu.
Tukutane Wiki ijayo kwenye
Michano inayojenga na si kubomoa inayotayarishwa na Rapa Mkola Man
mwenye chimbo lake Hale jijini Tanga, Ciao